KKKT MBEYA WAMUAGA ASKOF DK.MWAKYOLILE
√√Leo hii kanisa la kiinjli ni kirutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde wamefanya sherehe kubwa ya kumuaga aliyekuwa Askof mkuu wa Dayosisi hiyo DR.ISRAEL MWAKYOLILE ambaye anamaliza muda wake baada ya kuongoza dayosisi hiyo kwa muda wa miaka kumi na sita.
Gospel star Newz leo hii ilifanikiwa kuhudhulia katika sherehe hiyo iliyofanyika KKKT USHARIKA WA LUANDA kabwe jijini mbeya. Katika sherehe hiyo ambayo pia alisimikwa Askofu mpya wa Dayosisi hiyo DR.EDWARD MWAIKALI Iliongozwa na NAIBU SPIKA WA BUNGE DK.TULIA ACKSON MWANSASU akimuwakilisha Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.JOHN MAGUFULI ambapo ilihudhuliwa na jopo la maaskofu wa kanisa hilo pamoja na wachungaji wengi kutoka ndani na nje ya mkoa wa mbeya.
ASKOFU ISRAEL MWAKYOLILE alianza uchungaji mwaka 1986 akianzia katika kanisa la KKKT USHARIKA WA LUANDA MBEYA baada ya mika 14 aliteuliwa kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo akiwa amechunga makanisa mengi na hivi leo amemalizia KKKT USHARIKA WA TUKUYU MBEYA.
Imeandaliwa na JOHN MWAKIPESILE & JOSEPH MISHEY
©GOSPEL STAR NEWZ & MAGAZINE
TUPIGIE.0712688802 Kutangaza nasi kwa gharama nafuu sana.
MOJA YA PICHA ZA MATUKIO YA IBADA HIYO>>>>>>
Maoni
Chapisha Maoni